Sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja yazua hisia kali US

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waandamana kupinga sheria ya ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja mjini North Carolina

Maelfu ya wanaharakati walikutana katika bunge la North Carolina siku ya Jumatatu ambalo likikutana kwa mara ya kwanza tangu lipitishe sheria inayokosolewa kuwa dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.

Waungaji mkono pamoja na wanaopinga mswada huo walifanya mikutano tofauti nje ya bunge huko Raleigh.

Zaidi ya wakosoaji 50 wa sheria hiyo walikamatwa baada ya kuingia na kukataa kutoka katika jengo hilo.

Sheria hiyo yenye utata inatetea sheria inayowabagua watu wa jinsia moja.

Pia inawataka watu wa jinsia hiyo kutumia misala kulingana na vibali vya jinsia ya kuzaliwa.

Kampuni kubwa kama vile Benki ya Marekani na Apple zimekosoa sheria hiyo.