Haki miaka 26 baadaye kwa waliouawa Liverpool

Haki miliki ya picha PA
Image caption Haki miaka 26 baadaye kwa waliouawa Liverpool

Uchunguzi uliokuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu nchini Uingereza umeonyesha kuwa mashabiki 96 kwa klabu ya Liverpool, waliouawa wakati uwanja uliporomoka Kaskazini mwa Uingereza mwaka 1989, waliuawa kinyume cha sheria.

Uchunguzi huo wa miaka miwili wa janga la Hillsborough uligundua kuwa ukosefu wa usimamizi wa polisi na dosari kwenye mipangilio kulichangia kutokea kwa vifo hivyo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Pia ilitajwa kuwa tabia ya mashabiki haiwezi kuwa sababu.

Pia ilitajwa kuwa tabia ya mashabiki haiwezi kuwa sababu.

Jamaa wa famiia za mashabiki hao waliangua kilio mahakamani pindi kauli hiyo iliposomwa .

Watu waliokuwa wakifuatilia kusomwa kwa matokeo hayo kupitia kwa runinga kubwa nje walishangilia.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mashabiki 96 kwa klabu ya Liverpool, waliouawa wakati uwanja uliporomoka Kaskazini mwa Uingereza mwaka 1989

Janga hilo la Hillsborough la mwaka 1989 ndilo baya zaidi linalohusu spoti nchini Uingereza.