Mitsubishi yakiri kufanya udanganyifu tangu 1991

Haki miliki ya picha AFP Getty Images
Image caption Mitsubishi

Kampuni ya magari ya Mitsubishi imekiri kwamba imekuwa ikitumia ukaguzi bandia wa kiwango cha mafuta kinachotumiwa na magari hayo tangu mwaka 1991.

Hatua hiyo inajiri kufuatia ufichuzi kwamba kampuni hiyo imekuwa ikifanya udanganyifu katika data ya utumizi wa mafuta ya magari hayo kwa zaidi ya magari 600,000 yaliouzwa nchini Japan.

Makamu wa rais wa kampuni hiyo nchini Japan Ryugo Nakao amesema kuwa hajui ni magari mangapi zaidi yalioathiriwa.

Hisa za kampuni hiyo zilianguka zaidi kwa asilimia 10 mjini Tokyo siku ya Jumanne.