Mauzo ya simu za iPhone yashuka

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Apple

Kampuni ya Apple imeripoti kushuka kwa mapato yake kwa asilimia 13 katika robo ya pili ya mwaka siku ya Jumanne huku mauzo ya iPhone yakishuka.

Kampuni hiyo ya Teknolojia iliripoti kuanguka kwa mauzo yake kutoka dola bilioni 58 hadi dola bilioni 50.56 mwaka huu tangu mwaka 2003.

Mauzo ya simu aina ya iPhone yalishuka kutoka milioni 61.2 mwaka 2015 hadi milioni 51.2 katika kipindi kama hicho mwaka huu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mkurugenzi wa Apple Tim Cook

Mauzo nchini China yalishuka kwa asilimia 26,huku athari za sarafu ya dola iliozorota pia zikibainika.

Hisa za Apple zilianguka kwa asilimia 8.Hisa hizo zimeanguka kwa asilimia 20 katika kipindi cha miezi 12.