Hisa za Twitter zaanguka kwa asilimia 13

Haki miliki ya picha PA
Image caption Twitter

Mapato ya mtandao wa Twitter yamevunja matumaini ya wawekezaji wakati ambapo mtandao huo unajitahidi na ukuaji wa chini wa wateja na matangazo.

Hisa zilianguka kwa asilimia 13.6 wakati wa matokeo.

Mtandao wa Twitter ulikuwa na wateja milioni 310 kwa mwezi katika robo ya kwanza ya mwaka huku mapato yake yakiwa dola milioni 594.5.

Kampuni hiyo kwa miaka mingi imeshindwa kupata faida kutoka kwa wateja wake.

Mapato hayo yalidaiwa kuwa dola milioni 590 na dola milioni 610 ikiwa na kasoro cha kile ambacho wawekezaji walitarajia.