Al Jazeera yabanwa na serikali Iraq

Iraq Haki miliki ya picha AFP
Image caption Iraq imesema Al Jazeera imekiuka kanuni za uanahabari

Serikali ya Iraq imeliamuru shirika la utangazaji la Al Jazeera kufunga afisi zake mjini Baghdad.

Wanahabari wa shirika hilo pia wamepigwa marufuku kukusanya habari nchini humo.

Maafisa wa serikali wanasema shirika hilo la utangazaji limekuwa likikiuka kanuni za uanahabari, ambazo miongoni mwa mengine zinazuia mashirika ya habari kuangazia makundi ya waasi.

Shirika la Al Jazeera limesema limeshangazwa sana na hatua hiyo na limekanusha kuvunja kanuni zozote za kitaaluma.