Mvua kubwa: Mafuriko Tanzania na Kenya

Image caption Madhara ya mvua kubwa mjini Dar es Salaam

Leo imekuwa siku ngumu sana kwa uchukuzi mjini Dar es Salaam, Tanzania.

Kisa na maana,,,,mafuriko.

Image caption Wenyeji walitatazikika kuendesha shughuli zao za kawaida

Baadhi ya barabara kuu za kitovu hicho cha kibiashara cha Tanzania, zilikuwa hazipitiki.

Image caption Maji kila mahali

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha hivi sasa kanda yote ya Afrika Mashariki imesababisha mafuriko makubwa ambayo muundo msingi wa barabara za miji ya Nairobi na Dar es Salaam haziwezi kumudu.

Magari ambayo yalijaribu kutumia mabarabara ya Dar es Salaam yalikwama mengine huku yale yenye kimo cha juu yakifaulu kupita.

Image caption Magari mengi yamekwama barabarani

Wenyeji sasa wameanza kuhoji uwezo wa muundo msingi wa maji taka wa mji huo wa Dar es Salaam hususan ukizingatia kuwa ndio sasa msimu wa mvua umeanza.

Mtangazaji wetu wa Dar es Salaam Sammy Awami amefaulu kuondoka nyumbani kwake na katika pita pita zake ametutumia picha hizi zinazoonesha hali halisia ya baadhi ya mabarabara ya Dar es Salaam.

Image caption Wenye magari mjini Nairobi wataabika mabarabarani

Nchini Kenya hali sio tofauti.

Barabara ya kisasa ya Thika Super Highway haipitiki baada ya mvuo kubwa kunyesha mchana na kusababisha mafuriko makubwa.

Image caption Mtabiri wa hali ya hewa anasema mvua bado inatarajiwa

Kinaya ni kuwa mtabiri wa hali ya hewa anasema kuwa mvua kubwa inatarajiwa kunyesa mjini Nairobi na maeneo mengi ya nchi.

Wenyeji wa mji huo wa Nairobi wameanza kutoa hasira zao kwenye mitandao ya kijamii wengi wakipiga picha maeneo yaliyokumbwa na mafuriko.