Colombia yahalalisha ndoa za jinsia moja

Colombia Haki miliki ya picha AFP
Image caption Colombia ndiyo nchi ya nne kuhalalisha ndoa hizo Amerika Kusini

Mahakama ya Juu nchini Colombia imehalalisha rasmi ndoa za wapenzi wa jinsia moja nchini humo.

Hatua hiyo inaifanya Colombia kuwa nchi ya nne ya Amerika Kusini kuhalalisha ndoa hizo.

Wapenzi wa jinsia moja nchini Colombia awali tayari walikuwa wameruhusiwa kuungana na kuishi pamoja, na walipata manufaa mengi yanayohusiana na ndoa ikiwa ni pamoja na urithi, malipo ya uzeeni na marupurupu ya afya.

Lakini hawakuwa wameruhusiwa kufunga ndoa rasmi jambo ambalo sasa limefanyika.

Uamuzi huo ulitarajiwa kwa kiasi kikubwa baada ya uamuzi wa mahakama mapema mwaka huu wa kukataa pendekezo la kuwataka wathibitishaji wa mahakama kutosajili miungano ya wapenzi wa jinsia moja kama ndoa.