CIA yadai kuivuruga Al Qaeda

Haki miliki ya picha AFP
Image caption John Brennan mkurugenzi wa CIA.

Mkurugenzi wa CIA John Brennan amesema kwa miaka mitano iliyopita Marekani imeharibu kwa kiasi kikubwa kundi la Al Qaed baada ya kuuawa kwa kiongozi wake mkuu Osama bin Laden baada ya uvamizi wa vikosi maalum nchini Pakistan.

Bw Brennan amesema kuwa Bin Laden alikua nembo na mwenye mikakati imara na muhimu na ilikua lazima kumuondoa mtu huyo ambaye alihusika katika mashambulizi ya kigaidi mjini Washington na New York Septemba 11.

Haki miliki ya picha AP

Mkuu huyo wa CIA ameongeza pia kumuondoa kiongozi wa wa IS Abu Bakr Al-Baghdadi inaweza kuwa na athari kubwa.Lakini akaongeza kuwa vitendo vya kigaidi vinaathiri dunia nzima na changamoto hiyo itakua kwa miaka mingi ijayo.

CIA inasherekea miaka mitano tokea kuuawa kwa Bin Laden kwa kuelezea namna walivyofanikisha kukamatwa kwake kama jambo lililotokea siku za karibuni.