Lula da Silva ashutumiwa kwa ufisadi

Image caption Mwansheria mkuu wa Brazil, Rodrigo Janot

Mwanasheria mkuu wa Brazil,Rodrigo Janot,amemshutumu Rais wa zamani wa nchi hiyo Luiz Inacio Lula da Silva,kuhusika kwa kiasi kikubwa katika kashfa kubwa ya rushwa ya ufisadi inayoikumba kampuni ya mafuta ya Petrobras.

Janot amesema rushwa hiyo inayokadiriwa kugharimu dola za kimarekani bilioni mbiliisingeweza kutokea kama sio kuhusika kwa Rais Lula.Janot ameitaka mahakama kuu kuidhinisha uchunguzi dhidi yake pamoja na wanasiasa wengine 29,wafanyakazi wa umma sambamba na wafanyabiashara.

Rais huyo wa zamani wa Brazil,Luiz Inacio Lula da Silva amekanusha madai hayo.