Muhtasari: Habari kuu leo Jumanne

Miongoni mwa habari kuu leo, Leicester City mabingwa wapya wa EPL, upinzani Venezuela wawasilisha saini 1.8m za kura ya maoni na Whatsapp marufuku Brazil saa 72.

1. Leicester watawazwa mabingwa EPL

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ni mara ya kwanza kabisa kwa Leicester kutwaa ubingwa

Klabu ya Leicester City imeshinda taji la ligi kuu ya klabu bigwa ulaya ushindi ambao umetajwa kama historia katika kandanda. Leicester walianza kampeni zao za ubingwa huku wakipewa nafasi moja tu kati ya 5000 kushinda taji la ligi na pia wakitoka katika janga la kutaka kushuka daraja. Walipata ushindi hata bila kupiga mpira huku Tottenham waliotaka ushindi ili walitoka sare na Chelsea.

Mshambuliaji wa zamani Gary Lineker ambaye alitoka Leicester City amesema kushinda taji la ligi kuu ni mafanikio makubwa sana katika historia na haiwezi kusahaulika''

2. Upinzani wataka kura ya maoni Venezuela

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wapinzani wanasema Rais Maduro amechangia kudorora kwa uchumi

Upinzani nchini Venezuela umewasilisha sahihi za zaidi ya wapiga kura milioni 1.8 zinazoitisha kuandaliwa kwa kura ya maoni ya kumuondoa madarakani Rais Nicolas Maduro.

Hii ndiyo hatua ya kwanza ambayo itasababisha kufanyika kwa kura ya maoni ambayo itaandaliwa mwishoni mwa mwaka huu. Ili hilo kufanyika upinzani sasa ni lazima uwasilishe orodha nyingine ya majina millioni 4.

Wakosoaji wanalaumu sera za mrengo wa kushoto za Bw Maduro na mtangulizi wake Hugo Chavez kwa hali mbaya ya kiuchumi nchini Venezuela pamoja na uhaba wa chakula madukani.

3. Pwani ya Guinea hatari zaidi kwa meli

Ripoti mpya inaonyesha kuwa ghuba ya Guinea pwani mwa afrika ya magharibi imekewa eneo hatari zaidi duniani kwa mabaharia kwa sababu ya kuongezeka kwa idadi ya mashambulizi kutoka kwa maharamia.

Kulingana na utafiti uliofanywa na shirika moja la marekani unaonyesha kuwa maharami mara nyingi huteka watu ili kulipwa fidia.

Ripoti hata hiyo inasema kwa kikosi cha kimataifa cha wanamaji kimepunguza tisho kutoka kwa maharamia wa Kisomali nje ya pwani ya afrika masharikia baada ya maharamaia hao kushindwa kuteka meli mwaka uliopita wa 2015.

4. Whatsapp yafungiwa saa 72 Brazil

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jaji anasema Whatsapp ilikataa kufichua habari

Mfumo wa mawasiliano wa kutumia simu ya mkononi wa WhatsApp umekata rufaa dhidi ya uamuzi wa jaji nchini Brazil wa kufungwa kwake kwa zaidi ya saa 72.

Jaji Marcel Montalvao alisema kuwa kampuni hiyo ilikataa kufichua habari wakati wa uchunguzi kuhusu uhalifu.

WhatsApp ambayo inamilikiwa na Facebook inasema ilikuwa imetoa ushirikiano wake wote kwa mahamaka.

Mwezi Machi jaji Montalvao aliamrisha kukamatwa kwa afisa wa cheo cha juu wa Facebook kanda ya amerika ya kusini, kwa kukataa kushirikiana na uchunguzi kuhusu ulanguzi wa dawa za kulevya.

5. Kiongozi wa upinzani Brazil kuchunguzwa

Haki miliki ya picha Ag. Senado
Image caption Neves anatuhumiwa kupokea hongo

Mkuu wa sheria nchini Brazil ameiomba mahakama ya juu zaidi kuamrisha kuanza kwa uchunguzi wa ufisadi dhidi ya mwanasiasa maarufu wa upinzani Aecio Neves.

Seneta Neves, ambaye ni mgombea urais wa zamani amelaumiwa kuchukua hongo kutoka kwa kampuni ya nishati ya serikali.

Kesi hiyo inahusishwa na sakata kubwa ya ufisadi ambayo imekumba siasa za Brazil tangu mwaka uliopita.

Alishindwa mwaka 2014 na Dilma Rousseff ambaye anakabiliwa na uwezekano wa kumuondoa madarakani.

6. Mkimbizi aliyejiteketeza Australia ahamishwa

Mtafuta hifadhi raia wa Somalia ambaye alijiwasha moto katika kituo cha kuzia wahamiaji cha Australia kilicho katika kisiwa cha Nauru amepelekwa hospitalini mjini Brisbane.

Hodan Yasim mweye umri wa miaka 21 anakumbwa na majeraha mabaya.

Hicho ndicho kisa cha pili cha kujiwasha moto katika kituo cha Nauri chini ya wiki moja.

Mwanamme mmoja raia wa Iran aliaga dunia baada ya kujiwasha moto siku ya Jumatano mbele ya waakilishi wa umoja wa mataifa waliokuwa wamezuru kituo hicho