Aliyejaribu kuuza mwanawe ahukumiwa miaka 5

Haki miliki ya picha PA
Image caption Aliyejaribu kuuza mwanawe ahukumiwa miaka 5

Mahakama moja nchini Afrika kusini imemhukumu mwanamke mmoja kifungo cha miaka 5 kwa kujaribu kumuuza mwanawe kupitia mtandao wa kuuza na kununua wa Gumtree.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 20 atatumikia kifungo chake akiwa nyumbani kwa sababu mahakama hiyo iliona kheri impe fursa ya kumlea mwanawe.

Msemaji wa mamlaka ya mashtaka ya umma Natasha Kara, anasema kuwa manamke huyo alinaswa na mtego wa afisi yao baada ya afisa mmoja kujidai kuwa ni mteja.

Akijitetea mwanamke huyo aliiomba mahakama imhurumie kwani alizongwa na mawazo na ufukara baada ya mumewe kususia kumsaidia kumlea alipogundua kuwa hakuwa wake.

Hapo ndipo akaamua kumpeana, ila alikosa njia mwafaka na akalazimika kutumia mtandao huo wa kuuza Gumtree.