Justin Bieber ashtakiwa kwa kuvunja simu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Justin Bieber

Mwanamuziki Justin Bieber ameshtakiwa kwa dola milioni 100,000 kwa madai kwamba alivunja simu.

Nyota huyo ametuhumiwa kuivunja simu ya Robert Earl Morgan baada ya kujaribu kumrekodi Bieber wakati alipokuwa akinywa pombeKIsa hicxho kilitokea katika kilabu ya Cle mjini Texas mwezi uliopita.

Kulingana na mtandao wa TMZ,Justin Bieber alikasirishwa na kuchukua simu yake na kuivunja.

Thamani ya iPhone haifiki dola 100,000.

Lakini ameshtakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha kwa sababu simu hiyo ilikuwa na picha ambazo haziwezi kupatikana tena,ikiwemo picha za sherehe ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa bibi yake.

Morgan pia anadai kwamba alipoteza idad kubwa ya nambari zake za mawasiliano ya biashara.

Image caption Bieber akishikwa koo

Bieber bado hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.

Kisa hicho kinaaminika kufanyika jioni ambayo Bieber alionekana kumchoma na sigara Post Malone,ambay amekuwa akimsaidia katika ziara yake ya duniani.

Picha zilionekana siku chache baadaye zikimuonyesha Malone akiushika mkono wa Bieber kabla ya kumshika shingo Nyota huyo wa muziki wa Pop.

Lakini mwanamuziki huyo baadaye alisema kuwa walikuwa wakifanya utani.