Migiro ateuliwa balozi wa Tanzania Uingereza

Migiro Haki miliki ya picha Asha Migiro Twitter
Image caption Bi Migiro alihudumu kama Waziri wa Katiba na Sheria serikali iliyopita

Mmoja wa wanasiasa waliokuwa wakipigania tiketi ya kuwania urais kupitia chama cha CCM nchini Tanzania ameteuliwa kuwa balozi wan chi hiyo Uingereza.

Dkt Asha-Rose Migiro atachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw Peter Kallaghe ambaye amerejea nyumbani.

Anatarajiwa kuapishwa Alhamisi katika ikulu ndogo ya rais Dodoma.

Bi Migiro alihudumu kama Waziri wa Katiba na Sheria serikali iliyopita na alikuwa miongoni mwa wagombea watatu waliokuwa wamesalia kwenye kinyang'anyiro cha kuteua mgombea wa CCM uchaguzi wa mwaka jana, kabla ya mwishowe Dkt John Magufuli kuidhinishwa.

Mgombea huyo mwingine alikuwa Balozi Amina Salum Ali.