Papa Wemba azikwa

Image caption Papa Wemba enzi za uhai wake

Msanii nguli wa muziki nchini Kongo, Papa Wemba,amezikwa katika mji mkuu wa nchi hiyo kinshasa,baada ya siku tatu za maombolezo.

Maelfu ya waombolezaji walikusanyika kwa ajili ya ibada huku wakijipanga kando kando mwa barabara kuelekea makaburi yaliyopo nje kidogo ya mji.

Wemba alikua mashuhuri kwa mitindo yake ya kuvutia na yenye hisia iliyowavutia watu wengi kupenda muziki wake.Alianguka wakati akitumbuiza katika tamasha nchini Ivory Coast mwezi uliopita.