Syria uhalifu wa kivita waendelea

Haki miliki ya picha Reuters

Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amesema mashambulizi ya ndege za angani katika kambi ya wakimbizi,yanayohofiwa kuwaua zaidi ya watu 30 na kusema kwamba tukio hilo linapaswa kutajwa kama uhalifu wa kivita.

Mkuu wa kitengo cha haki za binaadamu katika umoja wa mataifa,Stephen O'Brien ametaka pawepo uchunguzi juu ya shambulizi hilo lililotokea katika jimbo la Idlib, karibu na mpaka wa Uturuki.

Raia nchini humo wanadai shambulizi hilo limefanywa na serikali,ambalo lililenga waasi katika eneo hilo wiki za hivi karibuni.Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza,Philip Hammond,amemtuhumu Rais wa Syria Bashar al-Assad,kwa kuonyesha dharau juu ya juhudi za kimataifa kumaliza mapigano nchini humo.

Ikulu ya Syria imeyetaja mashambulizi hayo kuwa yasiyoepukika.