Garang afurushwa katika kikao cha mawaziri

Image caption Mabior Garang ni mwana wa aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo John Garang

Waziri mpya wa maji nchini Sudan Kusini katika serikali mpya ya umoja amedai kwamba alifurushwa katika mkutano wa baraza la mawaziri kutokana na 'bow tie' yake.

Mabior Garang De Mabior alichapisha picha yake katika mtandao wa Facebook iliokuwa na maelezo yafuatayo:Nawasili nyumbani baada ya kufurushwa na rais Salva Kiir katika kikao cha baraza la mawaziri kwa kutovaa inavyohitajika.

Aliandika:Baada ya kurudi nyumbani na kubadilisha ''bow tie'' yangu kutokana na ushauri wa makamu wa rais Riek Machar nilirudi katika kikao hicho kabla ya walinzi wa Salva Kiir kunizuia kuingia.

Image caption Garang baada ya kubadilisha na kurudi katika kikao hicho

Bw Mabior ambaye ni mwandani wa aliyekuwa kiongozi wa waasi Riek Machar baadaye alisema hivi:Ni lazima waelewe kwamba serikali hii ya umoja haitakuwa kama ilivyokuwa awali.Mabadiliko yamekuja.

Serikali ya umoja iliapishwa wiki iliopita kulingana na makubaliano yaliolenga kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza Disemba 2013.