73 watekea katika ajali mbaya Afghanistan

Haki miliki ya picha
Image caption Abiria 73 wametekea hadi kufa katika ajali mbaya iliyohusisha mabasi mawili ya uchukuzi wa umma na lori la kubeba mafuta nchini Afghanistan.

Abiria 73 wametekea hadi kufa katika ajali mbaya iliyohusisha mabasi mawili ya uchukuzi wa umma na lori la kubeba mafuta nchini Afghanistan.

Msemaji wa wizara ya afya alieleza kuwa watu kama 70 walikufa...na kwamba wengi waliteketea na hawatoweza kutambulika.

Haki miliki ya picha
Image caption Abiri wengine walipelekwa hospitalini katika jimbo la Ghazni.

Wakuu wa Afghanistan wanasema kuwa idadi inazidi kuongezeka ya watu waliokufa katika ajali hilo lililotokea katika barabara ya mji mkuu wa Kabul kuelekea mji ulioko kusini wa Kandahar.

Abiri wengine walipelekwa hospitalini katika jimbo la Ghazni.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mohammadullah Ahmadi, mkurugenzi wa trafiki wa mkoa huo analaumu utundu wa madereva kwa ajali hiyo.

Ajali za barabarani ni kawaida nchini Afghanistan ambapo madereva wanamazowea ya kukaidi kanuni za barabarani na pia maafisa wa kuelekeza magari ni mwachache mno.

Mwandishi wa BBC aliyeko huko Mahfouz Zubaide anasema kuwa magari hayo matatu yalikuwa yanaendeshwa kwa kasi mno.

Haki miliki ya picha
Image caption Ajali za barabarani ni kawaida nchini Afghanistan ambapo madereva wanamazowea ya kukaidi kanuni za barabarani

Mohammadullah Ahmadi, mkurugenzi wa trafiki wa mkoa huo analaumu utundu wa madereva kwa ajali hiyo.

Anasema kuwa kwa jumla kulikuwa na abiria 125 katika mabasi hayo mawili.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Anasema kuwa kwa jumla kulikuwa na abiria 125 katika mabasi hayo mawili.

Msemaji wa idara ya afya Ismail Kawasi anasema kuwa itakuwa vigumu kuwatambua kwani walioteketea ,waliteketea kabisa.