Moto wawazidi maarifa wazima moto Canada

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Moto wawazidi maarifa wazima moto Canada

Maafisa wa Serikali ya Canada wamesema kuwa moto mkubwa, hatari na usioeleweka unatazamiwa kuvuka mpaka wa Mkoa masaa machache yajayo.

Wazima moto wanatarajia kuwa moto huo kuvuka maeneo yanayochimbuwa mafuta Kaskazini mwa Fort McMurray.

Maafisa hao wana hofu kuwa upepo huenda ukachochea moto huo na wakasema kuwa mvua kubwa isipotokea moto huo utateketea kwa miezi kadhaa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wazima moto wanatarajia kuwa moto huo kuvuka maeneo yanayochimbuwa mafuta

Mwandishi wa habari wa BBC ambaye ametembelea kambi kadhaa za muda ambazo zinakaliwa na walioondolewa makwao anasema kuwa wamepewa magunia ya vyakula, nguo na vifaa vya watoto kuchezea.