Trump: Kodi na mishahara kuongezwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Trump: Kodi na mishahara kuongezwa

Bwenyenye Donald Trump,anayetarajiwa kugombea kiti cha urais kwa urais kwa chama cha Republican ameonesha yuko tayari kubadilisha msimamo wake, kuhusu maswala makuu mawili ya uchumi - kodi na kiwango cha chini cha mshahara.

Akihojiwa kwenye televisheni, alisema matajiri wanafaa kutozwa kodi zaidi, ambayo ni kinyume na sera ya muda mrefu ya chama cha Republican.

Mwaka jana alisema atawapunguzia kodi matajiri.

Lakini sasa anasema, akichaguliwa kuwa rais, mipango yake itabadilika wakati wa majadiliano na baraza la Congress.

Aidha alisema kiwango cha chini cha mishahara kinafaa kuongezwa, lakini huo utakuwa uamuzi wa majimbo.