Dangote kuwasaidia waathiriwa wa Boko Haram

Dangote Haki miliki ya picha AFP
Image caption Dangote amewahi kutoa msaada awali kwa waathiriwa

Mtu tajiri zaidi Afrika Aliko Dangote ameahidi kutoa mamilioni ya pesa kusaidia waathiriwa wa mashambulio ya kundi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Ameahidi kutoa $10m (£7m) kuwasaidia waathiriwa hao.

Mfanyabiashara huyo ametoa tangazo hilo baada ya kuzuru kambi za watu ambao wamelazimika kutoroka makwao kutokana na mashambulio ya kundi hilo la Kiislamu.

Bw Dangote awali alikuwa ametoa dola milioni sita kama msaada kwa watu hao.

Haki miliki ya picha b
Image caption Dangote alitembelea kambi za wakimbizi

Miaka ya nyuma, wafanyabiashara wa Nigeria wametuhumiwa kwa kutotimiza ahadi wanazotoa za kutoa pesa za kuwasaidia waathiriwa.

Lakini afisa wa serikali nchini humo ameambia BBC kwamba, kwa mujibu wa ufahamu wake, Bw Dangote daima amekuwa akitimiza ahadi zake kwa waathiriwa.