Jaji aidhinisha kuhamishwa El Chapo

Haki miliki ya picha AP
Image caption El Chapo
Jaji ameamua kwamba mlanguzi mkubwa wa madawa ya kulevya Joaquin 'El Chapo' Guzman anaweza kusafirishwa hadi Marekani.

El Chapo alikamatwa Januari baada ya kuwa mbioni kwa miezi sita baada ya kutoroka kupitia mtaro kutoka gereza alimokuwa.

Siku ya Jumapili maafisanchiniMexico walimhamisha El Chapo hadi katika gereza lililo karibu na mpaka na Marekani.

Hatua hiyo imetokana na wasiwasi wa usalama, na sio kiashiria cha kusafirishwa hadi Marekani, kwa mujibu wa maafisa wa Mexico.

Lakini sasa jaji wa Mexico anasema mlanguzi huyo anaweza kusafirishwa hadi Marekani anakokabiliwa na mashtaka.

Hatahivyo, uhamisho wowote huedna ukachukuwa muda.

Mawakili wa El Chapo tayari wamekata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa kumsafirisha mteja wao na wizara ya mambo ya nje Mexico ina hadi siku 30 kuamua iwao kuidhinisha uhamisho huo u kuupinga.