Kenya yawakamata wanachama 36 wa al-Shabab

Haki miliki ya picha PSCU Kenya
Image caption Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Vikosi vya usalama nchini Kenya vinasema kuwa vimewakamata washukiwa 36 wa kundi la wanamgambo wa al-Shabab tangu mwezi Septemba mwaka uliopita kulingana na gazeti la The Star nchini humo.

Washukiwa hao walikamatwa katika msitu wa Boni mashariki mwa raifa hilo.

Miezi tisa iliopita ,jeshi lilizindua operesheni Linda Boni kuwafurusha wanamgambo walioaminika kujificha katika msitu huo.

Kenya imekabiliwa na mashambulizi ya wapiganaji wa al-Shabab,ikiwemo shambulio mnamo mwezi Aprili 2015 katika chuo kikuu cha Garissa lililowauwa watu 148.