UN yaisihi Kenya kutofunga kambi za wakimbizi

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption kambi ya wakimbizi ya Dadaab

Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia wakimbizi UNHCR limeitaka serikali ya Kenya kubatilisha msimamo wake wa kutaka kuzifunga kambi mbili za wakimbizi za Dadaab na Kakuma nchini humo.

Serikali ilisema Ijumaa iliopita kwamba kambi hizo mbili zitafungwa kufuatia wasiwasi wa usalama na ukosefu wa fedha.

Image caption Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa

Ilitoa tangazo kama hilo awali,lakini wakati huu serikali imesema kuwa inazifunga idare zake za wakimbizi katika kile kinachoonekana kama hatua ya kwanza ya kusitisha uhifadhi wa wakimbizi 600,000.

Wengi wao ni raia wa Somalia na Sudan Kusini.

Image caption Kambi ya Dadaab

''Tumelipokea na wasiwasi mkubwa tangazo hilo'',lilisema shirika hilo katika taarifa yake.Iliongezea:

La kushangaza ni kwamba hali ilivyo Somalia na Sudan Kusini inayowafanya raia kutoroka haijatatuliwa.