Rodrigo Duterte ashinda urais Ufilipino

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais mpya wa Ufilipino Rodrigo "Digong" Duterte
Meya wa jimbo aliyeongoza kampeni kali ya urais Ufilipino, Rodrigo "Digong" Duterte ameshinda uchaguzi huo kufuatia kujitoa kwa wapinzani wake.

Licha ya kwamba matokeo rasmi hayajatangazwa, mpinani wake mkuu Mar Roxas amekiri kushindwa baada ya kura zinazohesabiwa kudhihirisha Duterte anaongoza kwa kura nyingi.

Duterte amesema anakubali jukumu hilo kwa "unyenyekevu mkubwa".

Mgombea huyo aliye na umri a miaka 71 alizusha mzozo wakati wa kampeni kwa matamshi yake makali.

Ametaja ufanisi kutokana na msimamo wake mkali kutii sheria na kuimarisha utulivu.

Rekodi yake kama Meya asiyekubali uhalifu wa mji wa kusini Davao, ambao kwa wakati mmoja ulitambulika kwa kukithiri uhalifu, ulichangia Duterte kusifiwa kuwa muadhibu na sifa hiyo ilisambaa miongoni mwa wapiga kura.

Mambo yaliogubika kampeni za uchaguzi ni kukithiri kwa rushwa pamoja na umaskini na ukosefu wa usawa miongoni mwa ria aUfilipino licha ya ukuwaji wa uchumi ulioidhinishwa na rais anayeondoka Benigno "Noynoy" Aquino.

Matamshi makali ya Duterte dhidi ya uhalifu -- hata kutishia kuwaua wahalifu -- yanaonekana kuungwa mkono na wapiga kura wengi -- lakini yameshutumiwa na makundi ya kutetea haki za kibinaadamu.