Obama kuzuru mji wa Hiroshima

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mji wa Heroshima

Rais wa Marekani Barrack Obama anatarajiwa kutembelea Hiroshima mwezi huu akiwa ni rais wa kwanza aliyepo madarakani kufanya ziara ya mji huo wa Japan tangu ushambuliwe na bomu la kinyuklia la Marekani 1945.

Ziara hiyo itakuwa miongoni mwa ziara za bara Asia kuanzia tarehe 21-28 mwezi Mei ambayo pia itashirikisha Vietnam.

Bomu la Hiroshima mnamo tarehe 6 gosti mwaka 1945 liliwaua watu 140,000.

Pamoja na bomu la pili katika mji wa Nagasaki linasifika kwa kumaliza vita vya dunia vya pili.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hiroshima

Jimmy Carter amezuru Hiroshima lakini baada ya kukamilika kwa utawala wake.

Taarifa kutoka kwa Obama imesema kuwa rais atafanya ziara ya kihistoria huko Hiroshima na waziri mkuu Shinzo Abe ili kuangazia kuhusu ushirikiano uliopo wa kuleta amani na usalama katika dunia iliojaa zana za kinyuklia.