Uhaba wa chanjo dhidi ya homa ya njano

Haki miliki ya picha James Gathany CDC
Image caption Mbu wanaobeba homa hiyo huchangia kusambaa kwa wepesi katika nchi kama DRC
Wanasayansi Marekani wanaonya kuwa uhaba wa chanajo dhidi ya homa ya njano huedna ukazusha mzozo wa usalama wa afya.

Wahadhiri wakuu wawili wa chuo kikuu cha Georgetown University wamechapisha ripoti katika jarida la American Medical Association onyo kuwa mlipuko wa homa ya njano Angola huedna ikasambaa kimataifa.

Zaidi ya watu 270 wamefariki katika nchi hiyo iliopo kusini mwa Afrika tangu kuzuka mlipuko huo mwezi Desemba

Ugonjwa huo usio na tiba unaendelea kusambaa licha ya jitihada ya kuwapiga chanjo watuambao hawajaambukizwa.

Visa kadhaa vimeripotiwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Kenya na China. Uganda imeathirika na visa kidogo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kuna uhaba mkubwa wa chanjo

Mpaka sasa majimbo sita Angola ymeathirika, huku Luanda, ikiripoti zaidi ya visa 2,000 tangu kutangazwa mlipuko huo Desemba 2015.

WHO linasema chanjo zinakaribia kumalizika na lina wasiwasi kuhusu uwezekano wa kusambaa ugonjwa huo Congo.

Visa 37 vimeripotiwa vya watu walioingia nchini humo kutoka Angola.

Shirika hilo la afya duniani linasema hali ni lazima iangaliwe kwa umakini hususan katika mji mkuu Kinshasa sehemu iliyo na hali ya hewa sawa kama Angola na kunapatikana mbu wanaobeba homa hiyo ya njano pamoja na tumbiri wanaosambaza virusi.

Huchukua muda wa miezi sita kutengeneza chanjo kwa hiyo kuna pengo la muda kukabiliana na mlipuko mkubwa kama uliopo sasa Angola.