Huwezi kusikiliza tena

Cameron: Nigeria ni mafisadi wakuu duniani

Mzozo wa kidiplomasia unatokota baada ya Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, kunaswa kwenye Kamera akimwambia Malkia Elizabeth wa Pili kuwa viongozi wa mataifa mawili yenye ufisadi mkubwa kote duniani Nigeria na Afghanistan watakuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika kongamano la kupambana dhidi ya zimwi la ufisadi litakalofunguliwa siku ya Alhamisi mjini London.

Cameron: Nigeria ni mafisadi wakuu duniani

Matamshi hayo ya Cameron yalitolewa katika kasri la Buckingham bw Cameron alipokuwa amekwenda kumtembelea malkia Elizabeth katika sherehe ya kuadhimisha miaka 90 ya kuzaliwa kwake.