Princess Oyinbo
Huwezi kusikiliza tena

Muingereza anayeigiza filamu za 'Ogaa'

Je wewe ni mpenzi wa filamu za Nigeria maarufu kama Nollywood ?

Msanii mmoja wa kike raia wa Uingereza amekonga nyoyo za wapenzi wa 'Ogaa'' kwa kuigiza sauti na lahaja ya kingereza cha Pidgin inayotumika nchini Nigeria.

Ustadi wake katika lafudhi hiyo ya kiingereza imempa fursa ya kuigiza katika filamu kadhaa za Nollywood.

Mwelekezi mkuu wa filamu za ogaa, bw Lancelot Oduwa Imasuen, ametupa sehemu moja aliyoigiza Msanii Claire Edun, anayefahamika kwa mashabiki wake kama Princess Oyinbo.

Filamu hiyo ATM itazinduliwa ijumaa hii nchini Nigeria