Buhari hataki msamaha wa Cameron

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Muhammadu Buhari

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, ameuambia mkutano kuhusu vita dhidi ya ufisadi mjini London kuwa ahitaji msamaha kutoka kwa waziri mkuu wa uingreza David Cameron, kwa kuitaja nchi yake kuwa yenye ufisadi mkubwa.

Bwana Buhari amesema kuwa kile anachokitaka, ni kurejeshwa kwa mali iliyopatikana kwa njia ya ufisadi iliyo kwenye benki za Uingereza

Akiongea siku moja baada ya waziri mkuu wa uingereza David Cameroon kunaswa kwenye kamera akiitaja Nigeria kuwa nchi fisadi , Buhari alisema kuwa nchi yake inaongoza katika vita dhidi ya ufisadi.

Haki miliki ya picha
Image caption Muhammadu na Cameron

Alisema kuwa hatua mpya zimechukuliwa ikiwemo kubuniwa akaunti moja ya mapato yote ya serikali halutua ambayo itafnaya vigumu kwa mwamaziri kuiba pesa.

Amesema kuwa maelfu ya wafanyikazi hewa wameondolewa kutoka kwa vitabu vya serikali na shushuli haramu kwenye sekta ya mafuta zinakabiliwa.

Buhari aliuaambia mkutano wa nchi za madola mji London kuwa ufisadi ni tatizo la nchi zote na sio tu katika nchi zinazoendelea.