Rwanda ni mwenyeji wa WEF mwaka huu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wajumbe kutoka sekta ya biashara na serikali duniani wanakutana Kigali
Rwanda inaandaa kwa mara ya kwanza kongamano la uchumi duniani - World EconomicForum.

Kuna shughuli nyingi Kigali wakati kongamano hilo la mwaka hii linaanza Jumatano. Kauli mbiu ni "kushirikisha rasilmali za Afrika kupitia mageuzi ya kidijitali".

Zaidi ya wajumbe 1 200 kutoka kote duniani zaidi kutoka kitengo cha biashara pamoja na viongozi wa serikali watashiriki katika majadiliano ya kutathmini uwezo wa Afrika wakati dunia inaingia katika mageuzi ya nne ya kiviwanda.

Kwa mujibu wa WEF kikao hichi Rwanda kinanuia kutambua, kupatia umuhimu na kuchukua hatua kwa viongozi wa Afrika wakati wanaposhirikiana kujenga mataifa yao yanayoinukia kiuchumi katika soko linalozidi kuwa dijitali katika siku zijazo.

Serikali ya Rwanda inatarajia kuwa hili litaisaidia kuonyesha ina uwezo upi wakati pia inaadhimisha miaka 22 tangu mauaji ya kimbari ambapo zaidi ya watu 800 waliuawa.

Inataka dunia ijue kwamba rwanda ipo tayari kwa biashara.