Obama ataka shule ziheshimu wanaobadili jinsia

Image caption Rais Obama wa Marekani

Utawala wa rais Obama unazitaka shule kukubali wanafunzi wanaokumbatia jinsia tofauti na jinsia zao za kuzaliwa kutumia misaala ya kuogea ambayo ni sawa na hisia zao mpya.

Amri hiyo kutoka wizara ya elimu na ile ya haki zinaonya kuwa shule zitashtakiwa ama kukosa msaada iwapo zitapuuza amri hiyo.

Jaji mkuu nchini Marekani Loretta Lynch anasema kuwa kuwa agizo hilo linalenga kuwalinda wanafunzi kutobaguliwa pamoja na kunyanyaswa na wenzao.

Image caption Msaala wa watu waliobadili jinsia

Hatua hiyo inajiri wakati ambapo serikali ya kijimbo na jimbo la Carolina Kaskazini zinakabiliana mahakamani kuhusu sheria inayohitaji wanafunzi kutumia misaala ya kuoga ambayo inakumbatia jinsia zao katika vitambulisho vya kuzaliwa.