Paka mzee duniani anatoka Marekani

Image caption Scooter ndiye paka mzee duniani

Paka mmoja aliyezaliwa wakati wa utawala wa rais Ronald Reagan mwaka ametajwa kuwa paka mzee duniani.

Kitabu cha kumbukumbu za rekodi mpya cha Guiness book of World records kilisema kuwa Scooter alisherehekea mwaka wake wa 30 tangu kuzaliwa kwake mnamo tarehe 26 mwezi Machi.

Anaishi huko Mansfield,Texas.Mmiliki wake Gail Floyd anasema kuwa Scooter ameishi kwa miaka mingi kwa kuwa husafiri sana.

Image caption Scooter

''Kufikia sasa amezuru majimbo 45 kati ya 50 nchini Marekani.Miongoni mwa vitu anavyopenda kufanya vinashirikisha kuchanwa nyoya zake ,kuoga na kula kuku kila siku''.

Mmiliki wake Gail anasema alipokuwa mdogo,Scooter alipendelea kuchezea nywele zake na hata katika mabega yake na kutembea naye kila mahali alikotaka.

Bado anaendelea kumuamsha Gail kila asubuhi saa 12 asubuhi,ili kuzungumza, kuruka ruka na kila mara husubiri katika mlango wakati anapowasili kutoka kazini.

Image caption paka

Scooter amechukua taji hilo kutoka kwa mtangulizi wake, paka mwenye umri wa miaka 26 Corduroy aliyezaliwa tarehe mosi mwezi Agosti 1989 huko Oregon baada ya mmiliki wa Scooter Gail kutoa maelezo kwa wasimamizi wa kitabu cha rekodi mpya cha Guiness kwa ukaguzi.