Korea Kaskazini 'inaihami DR Congo'

Haki miliki ya picha AFP
Image caption DRCongo inatakiwa iarifu UN kuhusu ununuzi wowote wa silaha
Ripoti ya siri ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa ilioonekana a shirika la habari la Reuters inaarifu kuwa maafisa kadhaa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamesema kuwa Korea kazkasini imewapatia wanajeshi na polisi bastola.

Wamesema pia Korea Kaskazini wamewatuma wakufunzi 30 kutoa mafunzo kwa kikosi cha ulinzi wa rais na vikosi maalum.

Marufuku iliyoidhinishwa dhidi ya Korea Kaskazini kuuza silaha inaizuia kununua, kuuza na pia kutoa mafunzo.

Na marufuku dhidi ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo inaihitaji nchi hiyo kuiarifu kamati ya vikwazo katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa biashara yoyote ya kununua au kupokea mafunzo.

Wataalamu hao wanasema wamegundua kuwa maafisa kadhaa wa jeshi la Congo pamoja na maafisa wa polisi waiotumwa ng'ambo kama ujumbe wa Umoja wa Mataifa, wanaonekana kuwa na bastola hizo za Korea Kaskazini.