Kenya kujitetea mbele ya Wada wikendi

Image caption Hassan Wario

Ujumbe kutoka nchini Kenya utakaoongozwa na waziri wa michezo Daktari Hassan Wario utaelekea katika makao makuu ya shirika la kukabiliana na dawa za kusisimua misuli michezoni WADA nchini Canada wikendi hii, ili kuangazia hatua yake ya kulipiga marufuku shirika la kukabiliana na dawa hizo nchini Kenya ADAK, kwa kushindwa kuafikia mahitaji

Wario ameitaja hatua hiyo kama majuta makubwa lakini akasisitiza kuwa serikali ya Kenya itashirikiana na WADA kuhakikisha kuwa wanamichezo wa Kenya hawatumii dawa za kusisimua misuli.

Ameongeozea kuwa serikali itaimarisha juhudi zake kuhakikisha kuwa wanariadha wa Kenya wanashiriki katika mashindano ya Olimpiki ya Rio nchini Brazil.