Miliband: Fungeni kambi zote za wakimbizi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption David Miliband

Aliyekuwa waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza , David Miliband, ametoa wito wa kufungwa kwa kambi zote za wakimbizi duniani.

Bwana Miliband, ambaye ni rais wa kamati ya kimataifa ya uokozi,anasema kuwa wakimbizi wanafaa kufanywa raia wa mataifa wanamoishi na kupewa haki ya kufanya kazi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption kambi ya wakimbizi

Akiongea kabla ya kongamano la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadam, Miliband amependekeza asilimia kumi ya wakimbizi milioni 60 duniani, walio katika mazingira magumu, wapewe hifadhi na mataifa tajiri duniani.