Korea Kaskazini yazuia meli ya Urusi

Haki miliki ya picha EVN
Image caption jahazi

Mashua kutoka Urusi imezuiliwa na walinzi wa pwani wa Korea Kaskazini, katika Bahari ya Japan, ikiwa na watu watano.

Ripoti zinasema mashua hiyo ilizuiliwa wakati ilipokuwa inarudi Urusi, baada ya kushiriki kwenye mashindano ya mashua.

Wanabalozi wa Urusi wanataka watu waliokuwemo kwenye mashua hiyo waachiliwe huru haraka, na kwa sasa inaomba ruhusa ya kuwazuru.

Kawaida Urusi ni moja kati ya nchi chache, zenye uhusiano wa karibu na Korea Kaskazini.