Boris Johnson aifananisha EU na Hitler

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Boris Johnson

Mmoja wa wanakampeni wakuu wa kura ya maoni ya kuiondoa uingereza kutoka kwa muungano wa bara ulaya, meya wa zamani wa London Boris Johnson, ameufananisha muungano huo na viongozi katili wa zamani Napoleon Bona parte na Adolf Hitler.

Katika mahojiano na gazeti la Sunday Telegraph, bwana Johnson anasema kuwa wote wamekuwa na maazimio mabaya ya kuunganisha bara ulaya, japo akasema kuwa muungano wa bara ulaya umetumia mbinu tofauti.

Mwanasiasa huyo mhafidhina anasema majaribio kama hayo huishia kwa matokeo ya kuhuzunisha kwa kukosekana kwa msingi wa uaminifu kwa dhana ya bara Ulaya.