Mpaka wa Gambia na Senegal wazungumziwa

Image caption Gambia ni ardhi nyembamba iliyozungukwa na Senegal, isipokuwa mwambao wake wa magharibi, kando ya Bahari ya Atlantic.

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Senegal na Gambia wanazungumza, kujaribu kufumbua mkwamo mpakani, ulioendelea kwa miezi mitatu, na kusababisha upungufu wa bidhaa katika nchi zote mbili.

Madereva wa malori wa Senegal, walianza kufunga mpaka, pale Gambia ilipozidisha mara mia, ada ya kuvuka mpaka na kuingia nchini humo.

Baadhi ya madereva sasa wanafanya safari ya kilomita miatano, kuizunguka Gambia, ili kufika sehemu za kusini za Senegal.

Zamani wakichukua njia fupi ya kuvuka Gambia kufika kusini.

Gambia ni ardhi nyembamba iliyozungukwa na Senegal, isipokuwa mwambao wake wa magharibi, kando ya Bahari ya Atlantic.