Ndege kubwa zaidi duniani yatua Australia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Antonov An-225 Mriya ndiyo ndege refu na nzito zaidi kuwai kujengwa.

Maelfu ya watu nchini Australia wanaopenda ndege walikusanyika kutizama ndege kubwa zaidi duniani ya Antonov An-225 Mriya, ilipowasili mjini Perth nchini humo.

Ndege hiyo yenye urefu wa mita 84 na uzito wa tani 175 bila ya kubeba mzigo wala mafuta, ilikuwa ikisafirisha jenereta yenye uzito wa tani 117.

Misongamano ya magari ilifunga barabara wakati umati ulikusanyika kutizama kuwasili kwa ndege hiyo.

Ndege hiyo ilitoka mjini Prague na kusimama maeneo kadha mashariki ya kati na Asia, ikiwa safarini kwenda Australia.

Image caption Mikia yake miwli inaiwezesha ndege hii kubeba mizigo mizito.
Image caption Ngege hii ina jumla ya magurudumu 32 na injini sita
Image caption Antonov An-225 Mriya ilitoka mjini Prague na kusimama maeneo kadha mashariki ya kati na Asia, ikiwa safarini kwenda Australia.