Iran yawakamata wanaokiuka kanuni za dini

Haki miliki ya picha MEHR
Image caption Wale hujapisha picha kwenye mitandao ya kijamii bila kuvaa hijab hukamatwa

Utawala nchini Iran umewakamata watu wanane wanaofanya kazi na mashirika ya mitindo ambayo inatajwa kukiuka kanuni za dini ya kiislamu.

Kukamatwa huku ni sehemu ya oparesheni ya miaka miwilii ambapo wanamitindo wanalengwa hususan wale ambao huchapisha picha zao kwenye mtandao wa Instagram na mitandao mingine ya kijamii zikiwaonyesha wakiwa bila hijab.

Haki miliki ya picha FARS

Katika mahojiano ya runinga mkuu wa mahakama ya uhalifu wa mitandao mjini Tehran, amelamu mashirika ya mitindo kwa kuendeleza tamaduni zinazoenda kinyume na kanuni za kiislamu.

Amesema kuwa ni wajibu wa mahakama kuwachukulia hatua wale wanaokiuka maadili hayo kwa utaratibu unaofaa.