Mkutano wa kuzuia mgomo kufanyika Nigeria

Image caption Nigeria ndiye mzalishaji mkubwa zaidi wa mafuta barani Afrika

Serikali ya Nigeria inatarajiwa kufanya mazungumzo na vyama vikubwa vya wafanyikazi hii leo.

Hii ni katika jitihada za kuzuia mgomo unaopangwa kufanyika, kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta kwa asilimia 67

Chama cha wafanyikazi cha Nigeria Labour Congress (NLC) na cha Trade Union Congress (TUC) vimewataka watu kununua bidhaa za chakula kabla ya mgomo huo kuanza siku ya Jumatano.

Vyama hivyo pia vimetaka biashara na shule kufungwa siku ya mgomo.

Waziri wa mafuta nchini Nigeria Ibe Kachikwu amesema kuwa kupanda kwa bei, kutasaidia kumaliza uhaba wa mafuta na pia Nigeria itasalia kuwa nchi yenye mafuta ya bei ya chini zaidi barani Afrika.