Raia wa Rwanda afungwa maisha Sweden

Haki miliki ya picha THINKSTOCK
Image caption Mahakama za Sweden zinaweza kuwahukumu watu waliotenda uhalivu nchi za ng'ambo

Mahakama nchini sweden imemhukumu mwanamme mwenye umri wa miaka 61 kifungo cha maisha jela kwa kushiriki mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 .

Mahakama moja mjini Stockholm ilimhukumu Claver Berinkindi, ambaye ni raia wa Sweden kutoka nchini Rwanda, kwa mauaji , kupanga mauaji na kuteka nyara nchini Rwanda.

Hii inahusu kushiriki kwake kwenye mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 ambapo mshtakiwa alishiriki kama kiongozi,

Chini ya sheria za Sweden mahakama inaweza kuwahukumu watu waliotenda uhalivu nchi za ng'ambo.