Mtandao wa chakula wa BBC kufungwa

Image caption Mtandao wa chakula wa BBC

Mtandao wa chakula wa BBC ulio na risipi 11,000 za mapishi unatarajiwa kufungwa ikiwa ni miongoni mwa mipango ya shirika hilo kupunguza bajeti yake ya mtandao kwa pauni milioni 15.

Risipi zote za vya chakula hatahivyo zitawekwa katika kumbukumbu ijapokuwa mtandao wa biashara wa BBC Good Foof utasalia.

Mtandao wa habari wa shirika hilo hautafungwa lakini uamuzi kuhusu hatma yake utatolewa mwezi Julai.

Mapendekezo hayo yalitangazwa na mkuu wa maswala ya habari na matukio yanayojiri katika shirika hilo James Harding.

Mipango hiyo inashirikisha kufunga mtandao wa Newsbeat na programu pamoja na viasharia vya habari vinavyotoa habari kwa takriban maeneo 40 nchini Uingereza.

Huduma ya iPlayer itazifanya chaneli zisizo za runinga ya BBC na vipindi kuonekana kwa watazamaji.