Rais wa zamani azikwa Burundi

Image caption Mazishi ya Bagaza

Mazishi ya rais wa zamani wa Burundi Jean-Baptiste Bagaza ambaye aliaga dunia wiki mbili zilizopita yamefanyika kwenye mji mkuu Bujumbura.

Aliongoza kwa miaka 11 kutoka mwaka 1976 hadi mwaka 1987, na alifahamika kwa kuwa na msimamo mkali.

Mda mfupi kabla ya kupinduliwa, bwana Bagaza alipiga marufuku maombi yote ya umma siku za wiki. Makasisi wengine walikamatwa kwa kikuaka amri hiyo.

Bwana Bagaza pia alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya sasa.

Mkewe Fausta Bagaza amekuwa akiandika kwenye mtandao wa twitter, kuwaomba watu msahaba kwa mabaya mmewe alitenda.