Je, CIA imeingiliaje masuala ya Afrika?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption CIA ilipanga kumuua waziri mkuu wa kwanza nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Patrice Lumumba.

Ripoti kuwa kukamatwa kwa Nelson Mandela mwaka 1962 kulitokana na ufichuzi uliofanywa na ajenti mmoja wa shirika la ujasusi la Marekani CIA nchini Afrika Kusini, umesababisha kuwepo fikra kuhusu nyakati ambapo shirika hilo limelaumiwa kwa kuingilia kati masuala ya Afrika.

Kati ya masuala yaliyoangaziwa ni pamoja na kukamatwa kwa waziri mkuu wa kwanza wa Congo Patrice Lumumba mwaka 1961. Wabelgiji wameomba msamaha kwa kuhusika kwao lakini Marekani haijakiri kuhusika licha ya wajibu wa CIA kupanga kumuua.

Image caption CIA ilifahamu kuhusu mpango wa kumpindua rais wa kwanza wa Ghana Kwame Nkurumah.

Kupinduliwa kwa rais wa kwanza wa Ghana Kwame Nkurumah mwaka 1966. CIA ilifahamu kuhusu mpango wa mapinduzi na iliwasiliana na wapangaji wa mapinduzi.

CIA iliwaunga mkono vikosi vilivyokuwa vikipinga vile vya MPLA nchini Angola mwaka 1975, ambapo ilisaidia kwa kuwapa silaha na mafunzo waasi wa FNLA na wa Unita waliokuwa wakipigana na MPLA kuchukua udhibiti wa nchi baada ya kupata uhuru wake kutoka Ureno.

Image caption CIA ilsaidia vikosi vya Unita nchini Angola.

Walimuunga mkono Hissene Habre nchini Chad mwaka 1982, ambapo CIA iliunga mkono kupinduliwa kwa rais Goukauni Queddei kutokana na sababu kuwa Marekani iliogopa ushirikiano wa Libya na Chad kwa kumhusisha rais wa Libya Muammar Gaddafi.