Mauritius yaionya Uingereza kuhusu kisiwa

Image caption kisiwa cha chagos

Waziri mkuu wa Mauritania Sir Anerood Jugnauth ametishia kuishtaki Uingereza katika mahakama ya kimataifa kuhusu haki kuhusu uhuru wa kisiwa cha Chagos.

Ameliambia Bunge mjini Port Louis kwamba Uingereza ni sharti iiambie Mauritius mwishoni mwa mwezi Juni ni lini itakirudisha kisiwa hicho la sivyo ifikishwe mahakamani.

Kisiwa hicho kilikuwa katika eneo la Mauritius hadi mwaka 1965 wakati kilipochukuliwa na Uingereza na kukifanya eneo lake.

Image caption kisiwa cha Chagos

Uingereza baadaye ilikifanya kisiwa hicho kuwa kivyake ,na kuwafurusha wenyeji na kuiruhusu Marekani kutengeza kambi ya kijeshi katika kisiwa kimojawapo cha Diego Garcia.