Rais Mugabe awa babu Zimbabwe

Mugabe Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mugabe ameongoza Zimbabwe tangu 1980

Kiongozi wa muda mrefu wa Zimbabwe Robert Mugabe, 92, amekuwa babu rasmi.

Hi ni baada ya bintiye wa pekee Bona Chikore kujifungua mtoto mvulana katika hospitali moja nje ya nchi hiyo.

Bi Chikore alijifungua mtoto huyo mwezi uliopita, gazeti la serikali la Herald limeripoti.

Haki miliki ya picha RIA Novosti

Bw Mugabe amesema mkewe Grace kwa sasa yuko pamoja nab inti huyo wao na mjukuu wao na kwamba watarejea Zimbabwe mwezi ujao.