Madaktari wa Boston wafanikiwa kupandikiza uume

Haki miliki ya picha AP
Image caption Thomas Manning anaonekana mwenye furaha baada ya upasuaji

Hospitali moja mjini Boston imekuwa ya kwanza nchini Marekani kufanya upasuaji kupandikiza uume.

Thomas Manning mwenye umri wa miaka 64 alipatiwa kiungo hicho baada ya kugundulika kuwa uume wake uliathirika na saratani.

Madaktari wamesema zoezi hilo limefanikiwa na kumfanya Manning kuwa mtu wa tatu dunia nzima kufanyiwa upasuaji huo.

Mmoja wa madaktari waliofanya upasuaji huko Boston ni Dicken Ko, amesema wanaume wanaopoteza maungo yao hupata athari za kisaikolojia kwa kuwa ni maeneo nyeti yanayoathirika wengi wao hawapendi kufahamika hadharani.