Ri Yong-ho ateuliwa waziri wa mashauri ya kigeni

Image caption Ri Yong-ho

Korea Kaskazini imemteua Ri Yong-ho ambaye ni mpatanishi wa zamani wa masuala ya nuklia na balozi nchi Ungereza kuwa waziri wake wa masuala ya nchi za kigeni.

Ri Yong-ho ashahudumu kama mjumbe mkuu kwenye mazungunzo ya nuklia ya mataifa sita makuu duniani na pia alishiriki kwenye mazungumzo na marekani miaka ya tisini.

Mazungomzo hayo ya mataifa sita kuhusu mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini hayajawai kufanyika tangu mwaka 2008.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ri Yong-ho (kulia)

Barua iliyotumwa kwa Uingereza haikusema kile kilichofanyika kwa mtangulizi wake Ri, Ri Su-yong ambye anaaminiwa kupandishwa cheo.

Wadadisi wengine wanasema kuwa uteuzi huo ni dalili ya kujenga uhusiano, baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio lake la nne la nuklia na kurusha satellite na makombora kadha.

Hatua hiyo ilisabaisha nchi hiyo kuwekewa vikwazo zaidi kutoka kwa Umoja wa Mataifa na nchi zingine.